YANGA WAAMBULIA PATUPU KILA KIPENGERE TUZO ZA VPL


Mbali na Klabu ya Yanga kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzanilakini klabu  imejikuta ikiambulia  patupu kwenye tuzo hizo. Tuzo za  msimu wa 2019/20 ilitolewa hapo jana huku klabu ya Simba ikifunika kila kipengele ambacho wachezaji wake walitajwa.

Kabla ya tuzo hizo kutolewa ni mchezaji mmoja tu kutoka Yanga alifanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kiungo bora wa msimu ambacho kilikuwa kikigombaniwa na  Nicolas Wadada-Azam FC ,Clatous Chama Simba na Balama Mapinduzi kutoka Yanga. Hata hivyo Balama alifunikwa na Chama aliyeibuka kiungo bora wa msimu .

Kwa upande wa kikosi bora cha wachezaji waliofanya vyema hakuna mchezaji yeyote wa Yanga aliyeingia kwenye kikosi hicho ambacho klabu ya Simba ilitoa wachezaji 6 akiwemo Aishi Manula,Pascal Wawa,Miquissone,Kagere,Chama na nahodha John Bocco, Kagera walitoa wachezaji wawili ambao ni David Luhende na ,Azam FC mmoja ambaye ni Nicolas Wadada,Namungo walimtoa mchezaji mmoja ambaye ni  Lucas Kikoti  Costal Union ilimtoa Bakari mwamnyeto aliyejiunga na Yanga siku chache zilizopita.Post a Comment

0 Comments