BETI NASI UTAJIRIKE

WAFAHAMU WACHEZAJI 7 WANAOCHUKUA NAFASI YA MOLINGA,TSHISHIMBI NA MORRISON YANGA


Klabu ya Yanga imejipanga vyema kuelekea msimu wa 2020/21 baada ya kuweka nia ya kuwasajili wachezaji saba wa kigeni wenye viwango vya hali ya juu baada ya wale waliokuwepo klabbuni hapo kuonekana wabovu na wengine wakishindwa kuendania na mfumo wa mwalimu. Yikpe,Molinga,Morrison,Moro ,Niyonzima na Tshishimbi hawategemewi kusalia klabuni hapo.

Tetesi za wachezaji wanaotakiwa na Yanga 

 1. Mukoko Tonombe anayekipiga AS Vita ya DR Congo naye ni raia wa Congo ambaye inaelezwa kuwa huyu wameshafanya naye tayari mazungumzo.

2.  Eric Rutanga  anayekipiga Rayon Sports, naye anatajwa kumalizana na Yanga muda wowote anaweza kutua sawa na Tuisila Kisanda  wa AS Vita.

 3. Heritier Makambo yeye ni mshambuliaji naye anatajwa kuingia kwenye rada za Yanga ambapo kuhusu Makambo, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kwa kuwa anatajwa jambo lolote linaweza kutokea kwa sasa anakipiga Horoya AC.Makambo alicheza ndani ya Yanga msimu wa 2018/19 na alifunga mabao 17 ndani ya ligi. 

4. Yacouba Songne ambaye ni mchezaji huru pamoja na James Kotei ambaye amewahi kukipiga ndani ya Simba huyu inaelezwa kuwa tayari amemwaga saini ya miaka miwili ndani ya kikosi cha Yanga.

6, Yidha Sven kiungo anayekipiga ndani ya Kariobarg Sharks ya Kenya pia jina lake linatajwa kuwa kwenye rada za mabingwa hao wa kihistoria.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa hawatafanya makosa kwa msimu ujao kwa kuwa wamedhamiria kufanya usajili makini.

Post a Comment

0 Comments