VIUNGO WAWILI SIMBA BADO WAPO SANA HAWAENDI KOKOTE


Leo Agosti 18 klabu ya Simba imetangaza kuwaongezea mikatraba viungo wake wawili.Hassan Dilunga na Said Ndemla wamepewa mikataba ya miaka miwili kila mmoja kwa kazi nzuri walizofanya msimu wa 2019-20.

Said Ndemla hakupata nafasi mara kwa mara kutokana na uimara wa Jonas Mkude lakini mara kadhaa alipocheza alionyesha uwezo mkubwa na kufanya pengo la mkude lisionekane kwa mechi kadhaa alipokuwa majeruhi.

 Said Ndemla akilipokabidhiwa mkataba wa miaka miwili na kocha msaidizi wa Simba 

Hassan Dilunga kwa msimu wa 2019/20 alikuwa moto mkali. kabla ya kuwasili kwa miquissoine hakukuwa na mchezaji yeyote wa kumuweka benchi hivyo kumfanya awe na mabao 7 kwenye msimamo wa wafungaji bora wa ligi kuu. Ubora wake unamfanya aendelee kuwepo klabuni hapo

Post a Comment

0 Comments