Uongozi wa klabu ya Juventus umethibitisha kuachana na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Maurizio Sarri baada ya kudumu kwa msimu mmoja ndani ya klabu hiyo.Sarri aliibukia ndani ya Juventus akitokea Chelsea ambapo ndani ya msimu wa 2019/20 alifanikiwa kutwaa taji la Serie A ila kushindwa kwa timu yake kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kuishia hatua ya 16 bora kumemponza.
Kocha huyo mwenye miaka 61 licha ya uwezo wake mkubwa wa kufundisha bado hajawakosha mabosi wake wa Juventus jambo lililomfanya wamtimue mazima.
Kupoteza mbele ya Lyon kumewakasasirisha mabosi wa Juventus na kuamua kumfungashia virago.
Sababu haswa za Sarri kuondoshwa ndni Mchezo wake wa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Lyon alishinda kwa mabao 2-1 ila haikumpa nafasi ya kusonga mbele kwa kuwa mchezo wa kwanza alipoteza kwa kufungwa bao 1-0 kabla ya janga la Corona kuvuruga masuala ya ratiba zote duniani.
0 Comments