advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 24-08-2020


Leicester City inamuangalia beki wa kushoto wa Ajax, Nicolas Tagliafico, 27, kama mbadala wa Ben Chilwell, 23 ambaye anatarajiwa kujiunga na Chelsea. (Mail on Sunday)
Wolves wako tayari kumuuza winga Mhispania Adama Traore, baada ya Kocha Nuno Espirito Santo kuelezwa kuwa anapaswa fedha kwa ajili ya uhamisho. (Sunday Mirror)
Wolves wana mpango na winga anayekipiga Sevilla, Muajentina Lucas Ocampos, 26 kama mbadala wa Traore. (Sky Sports)
Manchester United wanaweza wakatoka kwenye mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu mshambuliaji Jadon Sancho, 20, na kurejea ndani ya mwaka mmoja. (Sunday Express)
Matumaini ya Manchester United kumsajili kiungo wa kati, David Brooks, 23, yameongezeka baada ya Bournemouth kukubali kuwa hawatamzuia mchezaji yeyote anayetaka kuondoka.(Sun on Sunday)
Arsenal inaamini kuwa itashinda mbio za kupata sahihi ya beki wa kati wa Lille, Gabriel Magalhaes, 22, lakini Manchester United imeitaka kambi ya mchezaji huyo kuchelewesha uamuzi .(Independent)
Simu na Kocha ya Mikel Arteta imemshawishi Magalhaes kujiunga washika bunduki. (Corriere dello Sport, via express.co.uk)
Jadon Sancho
Arsenal wanahitaji huduma ya Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara lakini wanahitaji mabingwa hao wa Bundesliga kupunguza dau la uuzwaji wa Mchezaji huyo . (Mail on Sunday)
Aston villa inatoa ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya mshambuliaji wa Celtic, Mfaransa Odsonne Edouard,22. (Sun on Sunday)
Barcelona wameandaa jibu kwa ajili ya mshambuliaji Lionel Messi, kuhusu ombi la uhamisho la mchezaji huyo, 32. (Clarin, via Mirror Online)
Arsenal na Barcelona wanamfuatilia kwa karibu mlinzi Malang Sarr, ambaye yuko huru baada ya kuondoka Nice. (Mail Online)
Kiungo wa Bayern Munich Thiago Alcantara
Newcastle, Everton, West Ham na Fulham wameonesha nia ya kumsajili beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling, 30. (90min)
Kocha wa Everton Carlo Ancelotti amezidi kukanganywa na mpango wa uhamisho wa klabu. (Star Sunday)
beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling
The Toffees wanamuuza mshambuliaji Richarlison, 23, kwa kitita cha pauni milioni 143. (Sunday Mirror)
Vilabu saba viko kwenye kinyang'anyiro kumnasa kiunga wa Liverpool, Mserbia Marko Grujic, 24. (Goal)
Mshambuliaji wa Valencia, 29, Rodrigo anapenda kuhamia Leeds United. (Mail on Sunday)

Post a Comment

0 Comments