Barcelona wanatumai kumshawishi kiungo wa kati Bernardo Silva, 25, aondoke Manchester City na wanaweza kumpatia ofa mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Ureno Nelson Semedo, 26, kama sehemu ya mkataba. (Telegraph - subscription required)
Mabingwa wa Primia Ligi Liverpool wanapanga kumuhamisha kiungo wa kati wa Wales David Brooks, 23, kwa pauni milioni 35 kufuatia kushushwa kwa daraja kwa timu ya Bournemouth. (Sun)
Everton, Tottenham na West Ham pia wanania ya kusaini mkataba na Brooks. (Star)
Mshambuliaji wa Bournemouth Joshua King analengwa sana na timu ya Ufaransa Paris St-Germain, huku hasimu wake wa Italia Lazio na Roma wakiwa wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 28. (Sun)
Uwezekano wa Tsimikas wa kuhamia Liverpool ni pigo kwa Leicester, ambao walikua wamempanga kama mchezaji atakayechukua nafasi ya Ben Chilwell, 23, iwapo kiungo huyo wa safu ya nyuma -kulia angeondoka kujiunga na Chelsea msimu huu. (Leicester Mercury)
Mshambuliji wa Burnley na New Zealand Chris Wood, 28, amepewa ofa ya kujiunga na Lazio. (Corriere dello Sport - in Italian)
Liverpool wamekubaliana na Olympiakos watoe gharama ya pauni milioni 11.75 kwa ajili ya kiungo wa safu ya nyuma-kushoto Kostas Tsimikas, 24, lakini bado hawajafikia makubaliano ya kibinafsi na mchezaji mwenyewe. (Liverpool Echo)
Lakini Tsimikas anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mine wenye thamani ya pauni 50,000-kwa wiki katika Anfield. (Guardian)
Sheffield United wanamatumaini ya kusaini mkataba na Mmmarekani anayecheza safu ya nyuma-kushoto Antonee Robinson fkutoka Wigan kwa pauni milioni 1.5 tu baada ya taarifa ya kushushwa kwa daraja kwa timu ya Latic kuthibitishwa. (Sun)
Arsenal wako tayari kulipa pauni milioni 18 zilizosalia kwenye mkataba na kiungo wa kati Mjerumani Mesut Ozil ambao unaisha mwaka ujao, au kumpatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 mshahara wa pauni 350,000- kwa wiki iwapo atahamia katika klabu nyingine (Mirror)
Mlinda lango Emiliano Martinez, 27, ameitahadharisha Arsenal kwamba anaweza kuondoka katika timu hiyo ili kupata muda zaidi wa mchezoili kuinusuru spot timu ya Argentina . (Continental, via Evening Standard)
Leeds inataka kusaini mikataba na wachezaji watano kwa ajili ya msimu ujao katika Primia Ligi, ikiwa ni pamoja ,ikiwa ni pamoja na Slavia Prague na kiungo wa msahambulizi ya kati wa Romania Nicolae Stanciu, 27, na kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Conor Gallagher, 20, ambaye acheza katika klabu ya Swansea nusu ya msimu uliopita. (Mail)
Kiungo wa kati wa Brazil Willian, 32, atasaini mkataba wa miaka mitatu na Arsenal, ambao unauwezekano wa wa kurefushwa kwa miezi 12, baada ya kuondoka Chelsea. (Telegraph - subscription required)
Kiungo wa kati-nyuma Mcolombia Yerry Mina, 25, amerejelea utashi wake wa kuhamia Everton huku kukiwa na tetesi juu ya hali yake ya baadae baada ya kubadili mawakala wake . (Liverpool Echo)
Kiungo wa zamani wa safu ya kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, amejiunga na klabu ya Lille lakini Muingereza huyo atacheza kwa deni msimu ujao katika klabu ya Ureno ya Boavista. (Guardian)
Juventus wameachana na mipango ya kusaini mkataba na Jorginho, 28, kutoka Chelsea na badala yake wanamlenga kiungo mwenzake wa kati Mtaliano Sandro Tonali, 20, kutoka klabu ya Brescia. (La Gazzetta dello Sport, via Mail)
Liverpool wamejipanga kusaini mkataba wa miaka mitano na kiungo wa nyuma-kulia Mwales Neco Williams mwenye umri wa miaka 19 (Goal)
Mkurugenzi wa mchezo Sevilla Monchi anasema kuwa itakua vigumu kwa upande wake kusaini tena mkataba na Mcroatia anayecheza safu ya kati Ivan Rakitic, 32, kutoka Barcelona msimu huu. (Diario de Sevilla, via Evening Standard)
Kiungo wa kati wa Manchester United Dylan Levitt yuko tayari kuachiliwa kwa mkataba kwa ajili ya msimu ujao, huku Mwales huyo mwenye umri wa miaka 19akiwa na uwezekano wa kuhamia katika klabu ya Championi . (Manchester Evening New
0 Comments