advertise with us

ADVERTISE HERE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAPILI TAREHE 9-8-2020


Chelsea inataka kuingiza pauni milioni 65 kwa kuwauza wachezaji wake ili kupata fedha za kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga West Ham Declan Rice.( Star)
Wakati huohuo kocha Frank Lapard amesema Chelsea ilijaribu kumbakisha winga Mbrazili Willian lakini ''hatakuwa na masikitiko '' iwapo ataamua kuondoka, huku mchezaji huyo, 31 akitarajiwa kujiunga na Arsenal kwa uhamisho huru mkataba wake utakapokwisha msimu huu. (Mirror)
Barcelona itatangaza ofa ya pauni milioni 14 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Manchester City, Mhispania Eric Garcia baada ya kuiambia timu yake kuwa hatatia saini mkataba mpya (Goal.com)
Eric Garcia ameiambia timu yake ya Manchester City kuwa hatatia saini mkataba mpya
Mwenyekiti wa juventus Andrea Angelo amekana kwamba mshambuliaji wa Portugal Christiano Ronaldo ataondoka katika klabu hiyo kufuatia kuondolewa kwao katika michuano hiyo na klabu ya Lyon ya ufaransa (Sky Sport Italia, in Italian)
Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Mjerumani Kai Havertz, 21, anaweza akawasili Chelsea mapema juma lijalo kwa ada ya pauni milioni 71, huku Bayern Munich ikiwa haina tena mpango na mchezaji huyo. (Star)
Klabu ya Ac milan imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay, 24 Lucas Torreira, ambaye kwa sasa nafasi yake ni finyu chini ya Kocha Mikel arteta. (Telegraph, subscription required)
Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Mjerumani Kai Havertz, 21, anaweza akawasili Chelsea mapema juma lijalo
Winga wa Watford Msenegali Ismaila Sarr, 22, yuko kwenye orodha ya wachezaji muhimu wanaotegemewa kusajiliwa na Liverpool. (Liverpool Echo)
Ajax inatazaia kumchukua winga wa Tottenham Hotspur Ryan Sessegnon, 20, kwa mkopo (Telegraph, subscription required)
Rennes wameanza mazungumzo kwa ajili ya kupata saini ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Chelsea, Fikayo Tomoro. (L'Equipe, in French)
Klabu ya Ac milan imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa Arsenal na Uruguay, 24 Lucas Torreira
Wolverhampton Wanderers wataanza mazungumzo ya mkataba na kocha Nuno Espirito Santo baada ya kampeni ya ligi ya Europa kumalizika. (Mail)
Manchester United inamuwinda mlinda mlango wa Napoli, Muitaliano Alex Meret ,23. (Star)
Everton inataka kumsajili kiungo wa Kati wa ufaransa na Atletico Madrid Thomas Lemar. Mchezaji Huyo mwenye umri wa miaka 24 hachezeshwi katika klabu hiyo ya ligi ya LA liga. (Le10 Sport, in French)
Tottenham wako kwenye mazungumzo na mchezaji wa nafasi ya ulinzi Milan Skriniar,25, ambaye pi anatolewa macho na Liverpool na Manchester United. (Tuttosport, in Italian)
Everton inataka kumsajili kiungo wa Kati wa ufaransa na Atletico Madrid Thomas Lemar
Leeds United wanafikiria uhaisho wa winga wa Liverpool na Wales Harry Wilson, 23, kwa ada ya pauni ilioni 15. (Sun)
Newcastle United inataka kumchukua Wilson kwa mkopo, ambaye msimu uliopita aliutumia kuchezea Bournemouth kwa mkopo, pia inamhitaji kiungo wa kati wa Chelsea Conor Gallagher, 20. (Northern Echo)
Crystal Palace itapambana na Fulham kupata saini ya kiungo wa kati wa Southampton Harrison Reed. Mchezaji huyo,25 , alicheza kwa mkopo Craven Cottage msimu uliopita. (Football Insider)
Harrison Reed
Mkurugenzi wa michezo wa Werder Bremen, Frank Baumann amesema klabu hiyo inayocheza Bundesliga ina mpango wa kumsajili kwa mkopo winga Mholanzi Tahith Chong ,20, anayekipiga Manchester United. (Manchester Evening News)
Arsenal, Juventus na Manchester City zinauwania kiungo wa kati wa Lyon Houssem Aouar,22. (L'Equipe via Mail)
Queen's Park Rangers wako ukingoni kuweka makubaliano na Tottenha kwa ajili ya kumsajili kwa mkataba wa kudumu kiungo Luke Amos, 23, ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo. (Talksport)

Post a Comment

0 Comments