BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 22-08-2020


Kocha mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumleta kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 29, Nou Camp. (Algemeen Dagblad, via Express)
Beki wa kati wa Lille na Brazil Gabriel Magalhaes, 22, amechelewa kufanya maamuzi ya mwisho ya kuelekea Arsenal baada ya Manchester United kuonekana kuwa na uwezekano wa kutoa kitita fulani kwa ajili yake. (Telegraph)
Manchester United imeonesha kunyamaza juu ya mpango wake wa makubaliano ya mkopo kwa winga wa Juventus na Mbrazil Douglas Costa, 29, na badala yake inafikiria kumsajili winga wa Bournemouth na Wales David Brooks, 23. (Manchester Evening News)
United imearifiwa kwamba ni lazima ilipe Bournemouth pauni milioni 40 kumsajili Brooks. (Sun)
beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot
Paris St-Germain inamnyatia beki wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 21. (O Jogo - in Portuguese)
Beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling, 30, anafuatilia kwa karibu makubaliano ya mkopo na Roma baada ya msimu uliopita kuwa Serie A. (La Gazzetta dello Sport, via Mirror)
Mazungumzo mapya ya mkataba kati ya United mlinda lango Mwingereza Dean Henderson, 23, yako katika hatua za mwisho. Makubaliano yao yanasemekana kuwa na thamani ya zaidi ya pauni 100,000 kwa wiki. (Sky Sports)
Beki wa kati wa Manchester United Chris Smalling
Liverpool inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara huku mchezaji huyo wa Uhispania, 29, akipatikana kwa pauni milioni 30. (Independent)
Mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, anataka kusalia Hornets, licha ya kushushwa daraja. (Talksport)
Tottenham inapanga kumsajili Ainsley Maitland-Niles, 22, wa Arsenal ambaye msimu uliopita alicheza kama mlinzi na kiungo wa kati kwa timu ya Arsenal. (Mail)
Liverpool inafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Thiago Alcantara
Brighton haitakubali ofa ya tatu ya Leeds kwa mlinzi Ben White, 22, na kusisitiza kwamba mchezaji huyo hauzwi. (Argus)
Kiungo wa kati wa Brazil Felipe Anderson, 27, anafikiria
Aston Villa iko tayari kutoa ofa ya pauni milioni 18 kwa mshambuliaji Mwingereza wa Brentford Ollie Watkins, 24, lakini upande wa mchezaji huyo unasemekana kushikilia kutaka pauni milioni 25. (Mail)


Real Betis inafanya mazungumzo na Brighton kuhusu uhamisho wa beki wa kulia wa Uhispania Martin Montoya, 29. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments