BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 15-08-2020


Washindi wa Ligi Kuu ya England Liverpool wamewasiliana na miamba wa Ujerumani Bayern Munich kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 29. (Bild, in German - subscription required).
Hata hivyo, Reds hawana mpango wa kumsaini mshambuliaji wa Vasco da Gama Mbrazil Talles Magno, licha ya tetesi zinazomhusisha kiungo huyo wa miaka 18- kuhamia Anfield. (Standard)
Mkuu wa soka wa Borussia Dortmund, Sebastian Kehl, amethibitisha kuwa mshambuliaji wa England Jadon Sancho,20, atasalia katika klabu hiyo licha ya kwamba ananyatiwa na Manchester United. (MEN)
Jadon Sancho
Maelezo ya picha,
United wako tayari kumenyana na Chelsea katika kinyang'anyiro cha kusajili beki wa kushoto wa Leicester City na England Ben Chilwell, 23. (Mirror)
Kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak,27, anatarajiwa kufanya uamuzi kuhusiana na hatima yake katika klabu hiyo japo Chelsea wanamtaka. (AS)
Arsenal wantatangaza usajili wa wa kiungo wa kimataifa wa Brazil Willian, 32, kwa mkataba wa miaka mitatu wikendi hii baada ya mkataba wa mshambulaji huyo kukamilika Chelsea. (Telegraph - subscription required)
Ben Chilwel
Maelezo ya picha,
Gunners wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Juventus na Atletico Madrid katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey,27. (Gazzetta Dello Sport, via Mail)
Kocha mpya wa Juventus Andrea Pirlo amemewafahamisha mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 32, na kiungo wa kati wa Ujereumani Sami Khedira, 33, kwamba wapo huru kuondoka klabu hiyo msimu huu wa jotor. (Goal)
Manchester United na Tottenham huenda wakapewa nafasi nyingine ya kumsaini mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 26, kutoka Juventus msimu huu wa joto. (Mirror)
Paulo Dybala
Maelezo ya picha,
Jadon Sancho anayelengwa na Manchester United "anafurahia sana" kucheza na kuelekeza timu ya kikosi ''maalum''cha Borussia Dortmund.
United itaitisha £20m kutoka kwa Roma ambayo inataka kumsajili beki wake wa safu ya kati na nyuma mwenye umri wa miaka 30- Chris Smalling, amabye yuko tayari kupunguziwa mshahara kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Italia maarufu Serie A. (Sun)
Napoli wako tayari kuafikiana na Everton kuhusu mkataba wa kumuuza kiungo wa kati wa Brazil Allan, 29. (Express)
Allan
Maelezo ya picha,
West Ham wanataka zaidi ya £80m kumuuza kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21, licha ya kiungo huyo kutakiwa na Chelsea. (Times - subscription required)
Mkurugenzi wa michezo wa Bayer Leverkusen Rudi Voller inasisitiza kuwa kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, anayenyatiwa na Chelsea, ataruhusiwa kuondoka klabu hiyo "chini ya hali fulani". (Kicker, via Standard)
Emerson Palmieri
Maelezo ya picha,

Beki wa Chelsea na Italia Emerson Palmieri, 26, amefikia mkataba wa kibinafsi na klabu ya Inter Milan. (Calciomercato, via Express)
Mahasimu wa Arsenal katika Ligi ya Primia, The Blues wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsaini beki wa kushoto wa Real Madrid Mhispania Sergio Reguilon, 23, kujiandaa kwa michuano ya Champion League. (AS - in Spanish)

Post a Comment

0 Comments