BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 13-08-2020

Gareth Bale hataondoka Real Madrid msimu huu na sasa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 32 yuko tayari kusalia Real kwa miaka miwili kabla ya kuhamia klabu mpya. (Mirror)
Aston Villa wanajiandaa kuweka dau la kumnunua mshambuliaji wa Brentford Ollie Watkins, 24. (Sky Sports)
Kingo wakati wa Manchester City Mhispania David Silva, 34, atajiunga na Lazio mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Guardian)
David Silva
Maelezo ya picha,
Klabu za West Bromwich Albion, Leeds na Fulham zilizopandishwa daraja katika ligi ya Primia zinawania kumsajili Ryan Fraser, 26, winga aliyeondoka Bournemouth mwisho wa msimu wa Juni kwa uhamisho wa bure. (90Min)
Chelsea wanapania kuiuzia AC Milan kiungo wao wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko, 25 na tayari wamepunguza bai yake kufanikisha mpango huo. (Sun)
Tiemoue Bakayoko
Maelezo ya picha,
Real Madrid hawana mpango wa kumuachilia kiungo wao wa kati Dani Ceballos, 24, kuondoka klabu hiyo atakaporejea nyumbani kutoka Arsenal. (AS)
Leicester City wameonesha nia ya kutaka kumnunua winga wa Burnley Dwight McNeil,20. (Sky Sports - via Leicester Mercury)
Mshambuliaji wa Leicester Kelechi Iheanacho, 23, ananyatiwa na klabu ya Uturuki ya Fenerbahce. (Fotospor - via Sport Witness)
Kelechi Iheanacho
Maelezo ya picha,
West Ham wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu mkataba mpya ambao utamfanya mshambuliaji Michail Antonio,30 kuwa mmoja wa wachezaji watakaolipwa donge nono. (Mail)
Mshambulijai wa Lazio, Ciro Immobile anadai kuwa Newcastle aliwasiliana na ajenti wake hivi karibuni kujadili uwezekano wake kuhamia Ligi kuu ya England. Mtaliano huyo wa miaka 30 hata hivyo ameahidi hataondoka Lazio. (Goal)
Mshambulijai wa Lazio, Ciro Immobile
Maelezo ya picha,
Klabu mbili za Ligi ya Primia na moja ya Bundesliga zinamtaka mchezaji nyota wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles. (Sky Sports)
Manchester United wanamlenga mshambuliaji wa Barcelona Mfaransa Ousmane Dembele wakimkosa Jadon Sancho, 20 kutoka Borussia Dortmund's. (ESPN)

Post a Comment

0 Comments