BETI NASI UTAJIRIKE

SPORT PESA NA YANGA WAJIPANGA KUNOGESHA WIKI YA WANANCHI DODOMA


Kampuni ya SportPesa wametoa msaada wa mipira na vifaa vya Michezo kwa shule jijini Dodoma ikiwa ni mkakati wa kusaidia kukuza mchezo wa soka kwa vijana.

"Mchezo wa soka ni ajira, sisi SportPesa tunaamini kwamba tukisadia vijana kukuza vipaji vyao tangu wakiwa chini tutatengeneza msingi na njia bora ya ajira yenye tija katika soka kwa vijana wetu hapo baadae," amesema Abbas Tarimba, Mkurugenzi wa Udhibiti na Uendeshaji wa Sportpesa Tanzania.
Amesema kwa kupitia tukio la Uzinduzi wa Sportpesa Wiki ya Mwananchi, la klabu ya Yanga leo Kampuni hiyo itashirikiana vyema na Klabu kuhakikisha mchezo wa soka unaendelea kutengeneza mazingira bora ya ajira ya ndani na nje ya uwanja kwa wananchi.


"SportPesa tutaendelea kurudisha sehemu ya faida tunayopata kwa jamii, kusaidia maendeleo yake katika nyanja mbalimbali, ikiwamo kwenye mchezo wenyewe wa mpira wa miguu," amesema.

Post a Comment

0 Comments