Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara klabu ya Simba wametikisa kwenye tuzo zilizotolewa na shirikisho la soka Tanzania kwa msimu wa 2019/20. Simba ilifnikiwa kuondoka na tuzo mbalimbali ikiwemo ya Kipa bora ambayo ilikwenda kwa Aishi Manula Meddie Kagere akitwaa tuzo ya mfungaji bora wa msimu baada ya kufunga mabao 22 ,Clatous Chama alitwaa tuzo mbili ikiwemo ya kiungo bora wa msimu pamoja na mchezaji bora wa msimu. Kocha Sven aliibuka kuwa kocha bora wa msimu baada ya kuip timu hiyo mataji mawili makubwa kwa msimu wa 2019/20. Kocha huyo aliiwezesha Simba kutwaa kombe la ligi kuu Tanzania Bara na lile la Azam Sports Confideration Cup. Klabu ya Simba iliondoka na kitita cha shilini milioni 100 baada ya kutwaa taji la ligii kuu Tanzania bara huku mshindi wa pili ambaye ni Yanga akikabidhiwa milioni 45,Azam wakiondoka na milioni 30 na Namungo Fc waliomaliza nafasi ya 4 walikabidhiwa kitita cha milioni 10 Shangwe ziliibuka kwa mashabiki wa Simba baada ya wachezaji wao 6 wakiingia kwenye timu bora ya msimu .Wachezaji hao ni Aishi Manula,Pascal wawa, Chama,Miquissone,Boko na Kagere.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments