Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema mabadiliko ya nembo ya klabu hiyo yalifanyika kulingana na mahitaji ya sasa
Mo amesema hawakukurupuka kubadili nembo, waliwashirikisha wataalamu mbalimbali mpaka kufanikisha zoezi hilo
"Kama klabu kubwa tulihitaji kuwa na logo iliyowazi na nzuri. Ukiangalia nembo yetu ya zamani, yule Simba wetu alikuwa mdogo, mpole, mzee lakini pia alikuwa haonekani vizuri.
"Sisi tumepitia nembo zaidi ya 1000, tumefanya utafiti na kazi hii imefanywa na wataalamu. Hatukutaka kuwa na mambo mengi kwenye nembo yetu kama walivyo wenzetu wana mpaka boxing"
"Tulichobadili sisi ni nembo tu, kauli mbiu imebaki vilevile," alisema Mo
Simba ilizindua nembo yake mpya hivi karibuni zoezi ambalo lilikwenda sambamba na uzinduzi wa jezi mpya kwa ajili ya msimu wa 2020/21
0 Comments