Inasemekana beki anayechezea Coastal Union Ibrahim Ame ameshamalizana na mabosi wa Simba ambao walikuwa wakisaka saini ya Bakari Mwamnyeto ambaye ametua ndani ya Yanga. Taarifa zisizo rasmi zinasema Yanga walikuwa kwenye mazungumzo ya mwisho kupata saini ya Ame ila kwa kuwa waliizidiwa ujanja na Simba wakaamua kuwajibu kibabe kwa kumalizana na Mwamnyeto. Coastal Union imejikuta ikiwapoteza mabeki wake muhimu ndani ya muda mfupi huku wakiwa na kazi ya ziada kuelekea msimu wa 2020/21.Kama uliifuatilia Coastal Union msimu wa 2019/20 utagundua wachezaji hawa walikuwa na maelewano mazuri Coastal Union imemaliza nafasi ya 7 kwenye msimamo imefungwa jumla ya mabao 30 ambayo ni machache kuliko yale iliyofungwa Namungo iliyo nafasi ya nne ikiwa imefungwa mabao 37. Habari kutoka ndani zinaeleza kuwa tayari Ame yupo kwnye ardhi ya Dar tayari kumalizana na mabosi wa Msimbazi.
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments