BETI NASI UTAJIRIKE

SENZO NI MWANANCHI KAMILI AKABIDHIWA MAJUKUMU MAPYA


Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla amemtambulisha Senzo Mazingisa kuwa miongoni mwa wataalam wanaosimamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa Uendeshaji klabu ya Yanga

Dk Msolla amesema Senzo atafanya kazi kama mshauri Mtaalam na tayari ameanza kushiriki vikao kati ya Yanga na La Liga

"Leo tunamtambulisha Senzo kama mshauri (Consultant) katika mchakato wa mabadiliko mfumo wa uendeshaji"
"Tunaamini uzoefu wake kwenye masuala ya uongozi wa soka utakuwa na mchango mkubwa kwetu. Ameanza kushiriki vikao na wenzetu wa La Liga na atafanya kazi nasi huku (Yanga) kama mshauri na pia atakuwepo kule GSM," alisema Dk Msolla

Aidha Bosi huyo wa zamani wa klabu ya Simba amesema amejisikia faraja kuwa sehemu ya wataalam watakaoshiriki kusimamia mchakato huo

"Nafurahi kujiunga na familia ya Yanga. Leo nimefarijika kupata nafasi ya kufika hapa Makao Makuu. Naamini kwa ushirikiano wetu tutaweza kufikia malengo," alisema
Jukumu langu kubwa ni kutoa ushauri wote muhimu kuhusu mabadiliko na kuunganisha hizi pande mbili kati ya Yanga na Laliga katika mfumo huu wa mabadiliko"
"Nitaanza kwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa na mahali pake ili tuweze kujenga timu nzuri yenye uwezo wa kushindana"
Sakata la Morrison

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Yanga Dk Msolla amesema leo wanawasilisha rasmi rufaa ya shauri linalomuhusu mchezaji Bernard Morrison Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS)
"Uamuzi wetu wa kuwasilisha malalamiko yetu katika Mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS kuhusu Bernard Morrison uko palepale, na leo tunawasilisha rasmi"

Post a Comment

0 Comments