Mzimbabwe Never Tigere amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kendelea na kazi katika klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam.
Mkataba huo utamfanya kuendelea kusalia kwa wababe hao wa Chamazi hadi mwaka 2022.
Tigere amekuwa na kiwango kizuri msimu uliopita, akisajiliwa kwenye dirisha dogo la usajili akitokea Platinum ya Zimbabwe, na kufanikiwa kufunga mabao manne katika Ligi Kuun ya Tanzania Bara, mawili kati ya hayo akitupia kwa mikwaju ya adhabu ndogo, na kuchangia pasi mbili.
Wakati huo Timu ya Azam FC itatambulisha kikosi chake cha msimu ujao kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC Jumapili kwenye Tamasha la Azam FC Festival Uwanja wa Azam Complex.
0 Comments