NANI AONDOLEWE KATI YA YONDANI,MAKAPU NA LAMINE MORO KUMPISHA BEKI HUYU


Klabu ya Yanga imefanikiwa kumnasa aliyekuwa beki kisiki wa Costal Union na Taifa Stars Bakari Nondo Mwamnyeto. Beki huyu amekuwa gumzo toka msimu wa 2018/19 huku kiwango chake kikipanda kila siku na kumfanya awe kivutio kwa klabu mbalimbali nchini.

Itakumbukwa tangu mwanzoni mwa msimu wa 2019/20 Mwamnyeto alikuwa akiwindwa na klabu za Simba ,Yanga na Azam lakini zote zilishindwa kumnasa kutokana na dau lake kuwa kubwa mno. 

Hatimaye Yanga imefanikiwa kumsajili beki huyo kimya kimya kwa mkataba wa miaka miwili na sasa ataitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2022. Kwa upande mwingine usajili Beki huyo umeibua maswali kwamba klabu ya Yanga ina utitili wa mabeki wa kati akiwemo Ally Ally,Said Makapu ,Lamine Moro,Dante na Kelvin Yondani je ni nani ataondoshwa kumpisha Mwamnyeto?

Kaimu katibu mkuu wa Yanga akiwa na Mwamnyeto walipokuwa wanasaini mkatabaPost a Comment

0 Comments