advertise with us

ADVERTISE HERE

MWENYEKITI ELIAS MWANJALA ATOA RIPOTI SAKATA LA MORRISON


Sakata la Benard Morrison na Yanga bado limekuwa gumu kutolewa maamuzi . Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji Elias Mwanjala amesema leo wameshindwa kufikia maamuzi ya sakata la mkataba kati ya Bernard Morrison na Yanga kutokana na moja ya nyaraka muhimu kushindwa kupatikana hivyo wataendelea tena kesho.
Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza mpaka sasa kesi yetu imefikia pazuri. kuna document moja kutoka kwa morson na kwa Yanga tumeziomba tunaamini kesho saaa nne tutaanza kikao Chetu na saa saba na nusu tutakuwa tumemaliza tutaanda utaratibu wa press conference kutoa maamuzi ya kamati"

Upande wa Simba ambao ni waajili wapya wa morrison wanaamini mchezaji huyo hakuwa na mkataba na klabu ya Yanga na hata suala la mkataba linalobishaniwa halina mashiko na kama Yanga watalazimisha mambo basi wao watalifikish suala hilo FiFA.

Upande wa Yanga ambao ni waajili wa zamani wa Morrison wanaamini mchezaji huyo ni mali yao na ana mkataba wa miaka miwili na mkataba wake unamalizika mwaka 22 julai 14. Mvutano huu unapelekea suala hilo kuibua sintofahamu kwa wadau wa soka nchini huku TFF wakitegemewa kutoa maelezo .

Post a Comment

0 Comments