Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amesema wameweka malengo ya kuhakikisha wanacheza hatua ya makundi ligi ya mabingwa msimu huu lengo kuu likiwa kutwaa ubingwa huo wa Afrika.Mo alizungumza na Wanahabari ofisini kwake akielezea mikakati ya mabingwa hao wa nchi
"Mimi siridhishwi na kushinda tu ubingwa wa ndani. Malengo yangu ni ubingwa wa Afrika. Malengo yetu sasa ni kuendelea kushindana ndani na kushinda ubingwa lakini pia kufika kwenye hatua ya makundi ya Ligi ha Mabingwa Afrika"
Aidha Mo amedokeza kuhusu ujenzi wa Hostel kule Bunju uwanja wa Mo Simba Arena pamoja na kuanzishwa kwa Academy
"Mipango yetu mwaka huu ni kujenga hosteli za timu, uwekezaji wa GPS ambao tutakuwa tunaona takwimu za wachezaji"
"Tutaanzisha akademi, kutakuwa na watu ambao watazunguka nchini kutafuta vipaji. Ambao watachaguliwa tutawaleta Dar na tutamgharamia. Tutakuza kipaji chake na tutamlipia gharama za shule."
Mo pia alizungumzia mchakato wa Mabadiliko ambapo amekiri bado haujakamilika lakini ameendelea kuipatia klabu ya Simba takribani Tsh Bilioni tatu kila mwaka kwa ajili ya kujiendesha
"Mfumo wa mabadiliko bado haujakamilika. Bilioni 20 zipo, kwasasa kila mwaka natoka bilioni 3 kama ruzuku kwa klabu. Naamini asilimia kubwa ya Wanasimba wananielewa."
Aidha Mo amesema siku chache zijazo watatangaza nafasi mbalimbali za kazi, moja ya nafasi hiyo ikiwa Mkurugenzi wa Ufundi.Amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kesho Simba Day akiahidi sapraizi nyingine
"Kesho kwenye SIMBADAY2020 kutakuwa na surprise haijawahi kutokea."
0 Comments