advertise with us

ADVERTISE HERE

MORRISON AFUNGUKA BAADA YA KUJIUNGA NA SIMBA ,ATOA NENO KWA YANGA


Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Benard Morrison amefunguka kwa mar ya kwanza tangu alipojiunga na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na FA klabu ya Simba. Morrison amesajiiwa kama mchezaji huru baada ya kumalizana na Yanga julai 14.

Morrison ameonekana kufurahia uhamisho wa kuitumikia Simba huku pia akishukuru uongozi wa klabu ya Yanga uliomleta nchini. Yanga bado wanamng'ang'ania mchezaji huyo wakisema alisaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo.

Morrion amenukuliwa akisema "Najua wengi wanasema kuhusu mimi mashabiki wanakasirika lakini hakuna baya, huu ni mpira na hii ni kazi yangu.
"Naiheshimu Yanga kwa kuwa ni timu kubwa na ina uwezo mkubwa nami pia ninajua kwamba Simba ni timu kubwa na ina mashabiki wake hivyo ni mwendelezo wa kazi,"

Post a Comment

0 Comments