BETI NASI UTAJIRIKE

MANULA ANAENDELEA KUWEKA REKODI ZA KIBABE LIGI KUU


Mlinda mlango namba moja wa Simba SC, Aishi Manula ameshinda tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2019/20.Manula ametangazwa mshindi wa tuzo hiyoIjumaa usiku Agosti 7, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kutokana na muendelezo wa ubora wa kiwango chake. Katika kinyang'anyiro hicho, Manula amewapiku Daniel Mgore kutoka Biashara United na Nourdine Balora wa Namungo ambao waliingia fainali. Katika mechi 18 za ligi msimu huu Manula hajaruhusu nyavu zake kutikiswa 'Clean Sheet' akiwa ndiye kinara kulinganisha na walinda milango wengine. Hii ni mara ya pili mfululizo Manula anachukua tuzo hiyo akiwa na timu ya Simba hali inayoonyesha kiwango chake kimekuwa kikipanda siku hadi siku.Manula amewahi twaa tuzo hiyo akiiwa mchezaji wa Azam

Post a Comment

0 Comments