MECHI ZA LEO: JE CHELSEA ATAIONDOA BAYERN MUNICH UEFA?


Klabu ya Chelsea inawakati mgumu sana siku ya leo kwenye mchezo wa raundi ya pili hatua ya 16 bora dhidi ya Bayern Munich. Mchezo wa kwanza Chelsea walikubali kipigo cha 3-0 uwanja wa Stamford Bridge na leo wapo Allianz Arena kumalizia mchezo wao

Ili chelsea aweze kupita moja kwa moja kwenda robo fainali ni lazima aifunge BayernMuich mabao 4-0. mchezo huo unategemea kuwa na mvuto wa aina yake. 

Mchezo mwingine ni Barcelona dhidi ya Napoli mchezo utakaopigwa Nou Camp jijini Barcelona. Barca wanatakiwa washinde mchezo huo kwa 1-0,2-1 ili waweze kwenda moja kwa moja hatua ya robo fainali kwani mchezo wa kwanza ulimalizika wa wao kupata sare ya 1-1 dhidi ya Napoli mchezo uliopigwa uwanja wa Napoli uitwao San Paolo stadium

Je nani ataingia robo fainali kati ya Bayern Munich,Napoli,Barcelona na Chelsea? Majibu ya maswali hayo yatapatikana jioni ya leo

Post a Comment

0 Comments