advertise with us

ADVERTISE HERE

MECHI KALI LEO>PSG VS RB LEIPZIG NANI ANAFIKA FAINALI LEO


Nusu fainali ya kwanza ya UEFA kati ya PSG dhidi ya RB leipzig itapigwa hii leo saa nne kamili usiku na mshindi wa mechi hiyo atakwenda moja kwa moja fainali kumsubiri mshindi kati ya Bayern Munich dhidi ya Lyon.

Habari njema ni kwa klabu ya PSG kwani kocha mkuu wa timu hiyo amethibitisha kwamba Kylian Mabppe amekwishaimarika na kunauwezekano wa kuanza kwenye mchezo huo. Kwa upande wa kipa Navas mambo bado hayajakaa sawa baada ya kuumia bega lake la kulia kwenye mchezo dhidi ya Atlanta.

PSG wamefika hatua ya nusu fainali baada ya kuiondoa Atlanta kwenye mchezo walioibuka na ushindi wa mabao 2-1.

RB Leipzig walifika hatua ya nusu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1  dhidi ya Atletico Madrid 

Mchezo huu unategemewa kuwa mgumu kwa pande zote mbili kwani utakuwa ni mara yao ya kwanza kufika hatua hii.

Swali lijnabaki ni nani atafika fainali kati ya PSG na RB Leipzig?

Post a Comment

0 Comments