MECHI KALI LEO: ETI MASHABIKI NANI KUONDOKA NA KOMBE LA FA ?


Fainali za kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kwa jina la FA zinapigwa kwa mara ya kwanza mjini Sumbawanga mkoani Rukwa. Mchezo huo wa Fainali unazikutanisha timu imara kwa msimu wa 2019/20.

Simba akiwa bingwa huku Namungo ikishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara. Klabu zote zimefika fainali baada ya kucheza michezo yao kwa ufanisi mkubwa. Namungo alifuzu fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sahare All Stars mchezo uliopigwa dimba la Mkwakwani jijini Tanga.

Kwa upande wa Simba wao waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya mahasimu wao klabu ya Yanga. Mchezo huu unategemewa kuibua hisia kwa mashabiki wa Soka nchini.Swali linakuja ni je nani atatwaa kombe hilo.

Historia kwa Ufupi 

Msimu wa 2019/20 klabu ya Namungo na Simba zimekutana mara mbili kwenye michezo ya ligi kuu Tanzania Bara. Mchezo wa kwanza Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 mchezo uliopigwa dimba la Taifa jijini Dar es salaam na ule wa pili ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya 0-0 dimba la Majariwa mkoani Lindi.

Siri ya Mchezo huo

1) SIMBA
Simba wasiuchukulie mchezo huo kimaskhara  a kudhani utakuwa rahisi kwani Namungo ya msimu huu haigusiki ,uwepo wa Bigirimana na Lusajo ni tishio kwa ngome ya Namungo lakini pia Namungo ya msimu huu imekuwa ikionyesha uwezo mkubwa baada ya kucheza na Yanga mechi mbili na kutoka sare zote ile ya (0-0) dimba la majariwa na ile ya 2-2 dimba la Mkapa. Namungo wamekuwa wakionyesha uwezo mkubwa hasa wanapokutana na timu kubwa za ligi kuu. Mfano  Walifungwa na Azam mchezo wa kwanza kwenye ligi kwa mabao 2-1 lakini waliifunga timu hiyo 1-0 mchezo wa marudiano.

2) NAMUNGO

Namungo wanakazi ya ziada kuelekea mchezo huo mgumu kwa pande zote mbili. Namungo wanatakiwa kuwa makini na wachezaji injini ya Simba ambao ni Miquissone,Chama na Kahata . Kama watataka kufanikiwa mchezo huo ni lazima wadhibiti eneo la kiungo ili kuibana Simba yenye washambuliaji makini kama Kagere na Bocco. 

Post a Comment

0 Comments