BETI NASI UTAJIRIKE

MCHAMBUZI MPYA ASHUSHWA AMOSPOTI MWENYEWE AFUNGUKA MIPANGO YAKE


Bw.Amos medeck mwenye (tisheti nyeupe) akiwa na mchambuzi mpya bwana Mohammed

Uongozi wa Amospoti umefanikiwa kumnasa mchambuzi nguli wa soka nchini Bw. Mohammed. Mohammed amekuwa ni mtaalamu wa kulichambua soka nje na ndani ya uwanja na alikwishafanya kazi na mchambuzi wetu bw.amos medeck . 
Kwa sasa Mohammed amekabidhiwa kijiti kipya ndani ya familia ya AMOSPOTI kama mchambuzi mkuu hivyo atachambua kabla na baada ya mechi lakini pia atahusika na kuwachambua wachezaji mbalimbali. 

Mkurugenzi mtendaji wa amospoti bw.Amos Medeck amenukuliwa akisema " Kwanza nafurahishwa na ujio wake,lakini pia nafahamu umahili wa Bw.Mohammed kwenye suala zima la mpira wa miguu,nimekwishafanya naye kazi kipindi cha nyuma na tumeona ni vyema akajiunga na familia yetu ya amospoti kuelekea msimu wa 2020/21.

Bw.Mohammed atahusika na masuala ya soka la kimataifa zaidi,na kwa umahili wake naamini atafanya mambo makubwa na amospoti itaendelea kutikisa anga la soka nchini"

Naye mchambuzi mohammed amenukuliwa akisema" Nipende kuushukuru uongozi wa amospoti kwa kunipa nafasi ya kujiunga na familia hii, watu wategemee mambo makubwa nje na ndani ya uwanja na  tumejipanga vyema kuelekea msimu wa 2020/21. Kwa leo sina mengi ila wadau waendelee kufuatilia amospoti

Post a Comment

0 Comments