Klabu ya Ruvu Shooting imepitisha panga la nguvu baada ya kuwaondoa wachezaji wake watano.Kocha Salum Mayanga alitoa mapendekezo kwa wachezaji hao watano kuondolewa kikosini huku akiitaka klabu hiyo kufany usajili wa uhakika kuelekea msimu wa 2019/20. Msemaji wa klabu hiyo Masau Bwire alitangaza majina matano ya nyota hao huku akiwahakikishia mashabiki wa timu hiyo kwamba lengo lao ni kujenga timu ya ushindani kwa msimu wa 2020/21 unaokwenda kuanza rasmi Septemba 06. Bwire alinukuliwa akisema"Leo Agosti 5 uongozi umekaa kikao na kuanza utekelezaji kwa ajli ya msimu ujao ili kuboresha kikosi chetu. "Wachezaji walioachwa ni pamoja na Zair Rajabu, Jamal Mnyate, Salum Makota, Edward Christopher na Adam Faraja,".
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments