Klabu ya Manchester United imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya robo fainali kombe la Europa League kwa msimu wa 2019/20. Manchester United waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lask huku wakimaliza raundi ya mtoano kwa uwiano wa mabao 7-1. Jesse Lingard alisawazisha bao dakika ya 57 kwa upande wa Manchester na Antony Martial aliipa Man United bao la ushindi dakika ya 88 huku lile la Lask likifungwa na Phillip. Kwa matokeo hayo Manchester United itakutana na Copenhagen ya Denmark hatua ya robo fainali. Kwa upande wa mechi nyingine ni Sharktar Donestic dhidi ya Wolfsbur mchezo uliomalizika kwa Shaktar kushinda mabao 3-0 na kuifanya timu hiyo kwenda robo fainali ikiwa na wastani wa mabao 5-1. Kwa upande mwingine Copenhagen wao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Istanbul na kuwafanya kufuzu hatua ya robo fainali wakikutana na manchester United mchezo utakaopigwa tarehe 10 Agosti. Romelu Lukaku na Eriksen wameibuka mashujaa kwenye mchezo dhidi ya Getafe baada ya kufunga mabao 2-0 n kuifanya timu hiyo kufuzu robo fainali
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments