BETI NASI UTAJIRIKE

MAMBO SITA USIYOYAJUA KUHUSU BAYERN MUNICH MSIMU HUU


Klabu ya Bayern Munich imeushangaza ulimwengu kwa kuibuka na ushindi wa mabao 8-2 dhidi ya Barceelona kwenye mchezo wa robo fainali ligi ya  mabingwa ulaya(UEFA CHAMPIONS LEAGUE)

Mabao ya Bayern yaliwekwa kimiani na Rhomas Muller mabao 2,Felipe Coutinho mabao 2 ,Robert Lewandowski bao 1,Perisic bao 1,Gnabry bao 1 ,Kimmich bao moja . Huku Barcelona ikipata mabao ya kufutia machozi kupitia bao la Alaba alilojiofunga na lile la Suarez.Mara baada ya mchezo huo kumalizika baadhi ya rekodi mpya zimeandikwa hii leo na baadhi kufikiwa na nyingine kuvunjwa. Haya hapa ni mambo manne ya kufahamu

1.Thomas Muller ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Bayern Munich kufunga mabao 6 kwenye michezo mitano waliyocheza.utakumbuka msimu wa 2014/15 hatua ya nusu fainali kati ya Barcelona na Bayern Munich bao la Muller liligeuka kuwa historia kwenye mchezo ule na kuingia kinyang'anyiro cha bao bora la wiki.

2.Bayern Munich wamefunga mabao 39 kwemichezo 9 waliyocheza msimu huu. Katika michezo yote hawajafungwa wala kutoa sare mchezo wowote na waliweka rekodi ya kufikisha pointi 18 hatua ya makundi.

3.Kwa msimu wa 2019/20 Bayern Munich wamefanikiwa kufunga mabao 152 kwenye michuano yote wakivunja rekodi waliyoiweka msimu wa 2012/14 walipofanikiwa kutwaa makombe matatu msimu mmoja kwa kufunga mabao 151 michuano yote.

4.Bayern Munich wamefanikiwa kuivunja rekodi yao waliyoiweka msimu wa 2014/15 walipoifunga porto FC mabao manne ndani ya dakika 36 na wamefanya hivyo kwa kufunga mabao manne ndani ya dakika 31 dhidi ya Barcelona.

5.Felipe Coutinho anakuwa mchezaji wa kwanza wa Barcelona aliyetolewa kwa mkopo kwenda Bayern Munich na kuifunga timu hiyo mabao mawili kwenye hatua ya robo fainali . Couintho msimu huu amefunga mabao 8 kwenye mechi 23 alizocheza hiki akitengeneza mabao 6. Kwa msimu wa 2019/20 amefanjikiwa kutwaa kombe la German Champion pamoja na German Cup winners.

6. Robert Lewandowski amefanikiwa kuweka rekodi mpya baada ya kucheza michezo 8 huku akifunga michezo 8 mfululizo na kubwa zaidi ni kufikisha mabao 14 kwenye mechi 9 alizocheza . Msimu 2019/20 anauwezekano mkubwa wa kuondoka na kiatu cha mfungaji bora wa uefa kwani mpinzani wake wa karibu Erling Halaand mwenye mabao 10 amekwishatolewa kwenye michuano hiyo.

Post a Comment

0 Comments