advertise with us

ADVERTISE HERE

MAKALA:MASWALI MATATU WANAYOPASWA KUJIULIZA AJIBU,GADIEL MICHAEL NA KAKOLANYA


Swali la kwanza wanalopaswa kujiuliza akina Ajib ,Gadiel Michael na Beno Kakolanya ni kuwa kwanini walisajiliwa na Simba? Au kwanini wapo Simba? Malengo yao ni yepi kisoka ? na wanataka kufika wapi baada ya mikataba yao kumalizika?

Haya ni maswali wanayopawa kujiuliza nyota hawa waliokuwa tegemezi kwa klabu ya Yanga msimu wa 2018/19. Chini ya Mwinyi Zahera wachezaji hawa walikuwa ni kila kitu ,ilikuwa ni lazima waanzishwe kikosi cha kwanza na bila wao Yanga ilikuwa nyepesi tu kufungika.

Utakumbuka mabao 10 ya Ajibu na zile pasi za 17 aizotengeneza kwa msimu ule , utakumbuka umahili wa Gadiel Michael pale upande wa kushoto ilikuwa ni lazima mshambuliaji ujipange haswa kumpita beki huyu.  Vipi kuhusu umahili wa Kakolanya pale langoni? Unakumbuka michomo aliyoikoa kwenye ule mchezo wa watani uliomalizika kwa sare ya 0-0.

Wachezaji hawa msimuwa 2019/20 walisajiliwa kwa mbwembwe pale msimbazi. Kwa tuliokuwa na jicho pevu tuliona jinsi nyakati zao zinavyokwenda kumalizika kwa kukaa benchi. Leo hii ukitajiwa jina la Ajib , Gadiel au hata kakolanya utawaweka kundi la Average Player yaani wachezaji wa kawaida na hiyo ni kutokana na kushindwa kuonyesha umahili wao kwa kila mechi walizopangwa. 

Kakolanya ilikuwa ni lazima afungwe walau bao moja kwenye kila mchezo alioucheza, Gadiel amejikuta akiishia benchi mbele ya Mohammed Hussein na hata Ajibu kawa na wakati mgumu mbele ya Chama ,Kahata ,Shiboub na hata Fraga.

Ikumbukwe wachezaji hawa wamesaini mikataba ya miaka miwili na swali linakuja ni lini wataonyesha umwamba wao ndani ya Simba? kama watashindwa kuonyesha msimu wa 2020/21 basi tusitegemee kuwaona ndani ya Simba msimu wa 2021/22 maana watakuwa ni average player .

Haya ni maswali manne kwa nyota hawa wanayopaswa kujiuliza

1. Tupo Simba kukuza viwango vyetu ili kesho tuendelea kubaki kwenye historia ya ligi kuu Tanzania bara au tupo Simba kulipwa mishahara minono kutoka kwa Mo Dewji

2. Baada ya mikataba yetu kumalizika tutatakiwa kuondoka hapa je tutaenda timu gani? na tutalipwa vyema zaidi ya hapahuko tunakokwenda?

3. Vipi nafasi zetu kwa timu ya Taifa inayoshiriki Chan,Afcon na kufuzu kombe la dunia  tutapata wasaa wa kuitumikia timu hiyo?
Post a Comment

0 Comments