BETI NASI UTAJIRIKE

MAJINA YA MAKOCHA WANAOITAKA NAFASI YA LUC EYMAEL YANGA YAVUJA


Klabu ya Yanga imepokea CV za makocha zaidi ya 60 wanaotaka kurithi nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Lucy Eymael. Uongozi wa Yanga umesema ndani ya wiki mbili zijazo utamtangaza kocha atakayekinoa kikosi hicho kwa msimu wa 2020/21 huku majina kadhaa yakitajwa ambayo ni Hans Pluijm,Thiery Hitimana ,Ernie Brands,Patrick Aussems, na Mecky Mexime.

Moja wa viongozi wa Yanga amenukuliwa akisema
  "Ndani ya wiki mbili hizi kocha mkuu mpya wa Yanga atajulikana baada ya kumfukuza Eymael hivi sasa uongozi unapitia CV za makocha mbalimbali waliotuma maombi kuja kuifundisha timu,"

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Simon Patrick hivi karibuni alinukuliwa akisema kuwa:"Tutahakikisha tunafanya uamuzi sahihi kwa kuteua kocha atakayetufaa kutokana na ukubwa wa Klabu ya Yanga, "

Post a Comment

0 Comments