BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI: JE NI WAKATI SAHIHI KWA KAKOLANYA KUONDOKA SIMBA



Kuna uwezekano kipa namba mbili wa klabu ya Simba Beno Kakolanya anaweza kutimkia azam. Kipa huyo tangu amejiunga na Simba msimu wa 2019/2020, ameonekana kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

Siku chache zilizopita Kakolanya alitofautiana na kocha wake wa makipa, Mohammed Mwalami baada ya kumuondoa kwenye msafara wa timu hiyo uliokwenda mkoani Tanga kucheza mchezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union Julai 23 kwa kile alichodai ana majeraha wakati yeye ni mzima.

Kwa mujibu wa taarifa sizizo rasmi Kakolanya anatajwa kwenda Azam kuchukua nafasi ya kipa Mghana, Razak Abarola ambaye ameachwa na timu hiyo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kipa mwenyewe Kakolanya ndiye aliyeomba kuondoka Simba na kwenda Azam baada ya kuonekana hana maelewano mazuri na kocha wake wa makipa, pia kupoteza nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

“Yapo mazungumzo ya siri yanafanywa kati ya uongozi wa Simba na Azam waliomuomba kipa huyo kwenda kuichezea timu hiyo huku wakipanga kununua mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha Kakolanya.

“Kakolanya anaonekana hana furaha tangu alipojiunga na timu hiyo, hiyo ni baada ya kuonekana kushindwa kumtoa Manula katika kikosi cha kwanza kabla ya kuomba kuondoka mwenyewe.

“Kitendo cha yeye kutopata nafasi ya kucheza kimemfanya akose furaha ndani ya timu hiyo, hivyo akaona ni bora akaondoka hapo na kwenda kwingine kucheza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alipotafutwa Kakolanya ambaye alikuwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Namungo FC kwa njia ya simu kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

Post a Comment

0 Comments