BETI NASI UTAJIRIKE

KUMBE HUYU STRAIKA ALIYESAJILIWA NA YANGA ANABALAA


 Aliyekuwa mshambuliaji bora wa kikosi cha Mbao FC Waziri Junior amemwaga rasmi wino wa kuwatumikia mabingwa wa kihistoria klabu ya Yanga.Junior amesaini mkataba wa miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika ndani ya Mbao FC.

Wazir alikuwa na msimu mzuri baada ya kufunga mabao 12 na alikuwa ni namba moja ndani ya kikosi hicho.Mchezaji huyo alimalizana Mbao FC Agosti Mosi, kwenye mchezo wa play off dhidi ya Ihefu kwenye mchezo wa playoff uliochezwa Uwanja wa Kirumba ambapo alifunga mabao mawili.


Wazir Junior amewafunika mastraika wote wa Yanga msimu huu kuanzia Molinga mwenye mbao 10 ligi kuu, Ditram Nchimbi ,Yikpe na Tariq.Kwa maana nyingine kama Wazir angekuwa mchezaji wa Yanga msimu wa 2019/20 basi angekuwa ni top score

 Mbao FC wameshuka daraja na watashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2020/21.Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Yanga msimu huu. walianza na Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar akafuata kwa Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini  Mustapha wa Polisi Tanzania.


Post a Comment

0 Comments