BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA NAMUNGO AANZA KUJITETEA KUELEKEA FAINALI DHIDI YA SIMBA LEO


Kocha Mkuu wa Namungo FC Thiery Hitimana amesema kuwa ana kazi ngumu leo mbele ya Simba ila anaamini watapambana kupata matokeo.Namungo inashuka dimbani dhidi ya Simba kwenye mchezo wa fainali za ASFC mchezo utakaopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga 
Thiery amesema kuwa wanatambua kazi itakuwa ngumu kwa kuwa wanacheza na mabingwa wa Ligi Kuu Bara.
"Ukiwa unacheza na bingwa lazima uingie kwa tahadhari kubwa na akili kichwani kwani fainali siku zote ni fainali haina wepesi lazima itakuwa ngumu.
"Ninawaheshimu wapinzani wangu kwa kuwa nimewahi kukutana nao licha ya kwamba wachezaji wangu wengi ni wagonjwa tutafanya vizuri," amesema.

Namungo ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya kushinda hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0 mbele ya Sahare All Stars mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Kuna uwezekano mtaalmu wa mabao Edward Manyama akakosa mchezo wa huo  kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaoumwa.

Post a Comment

0 Comments