Kocha mkuu wa Namungo FC Thiery Hitimana amesema kwa sasa anaandaa ripoti ya msimu 2019/20 ili aweze kujua hatma yake ndani ya kikosi cha Namungo FC . Kocha huyo amekuwa na mafanikio kwani aliiwezesha timu hiyo kushika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi huku akifika fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup mchezowalioupoteza kwa kipigo cha mabao 2-1.Na kuifanya timu hiyo kupata nafasi kushiriki michuano ya kombe la shirikisho Africa. Kocha huyo amekuwa akihusishwa kutua Yanga mara baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Luc Eymael kutimuliwa mwezi Julai akihusishwa na kashfa ya kauli za kibaguzi alizozitoa kwenye mchezo dhidi ya Lipuli. Hitimana amenukuliwa akisema "Endapo nitsalia ndani ya Namungo sitaongeza nyota yoyote wa kimataifa , Ripoti yangu itasema ni mchezaji gani namtaka na mahitaji kwa kikosi. Kwa sasa sitaweka wazi mpaka viongozi waone ripoti yangu na wafanyie kazi Kocha huyo Mrwanda ameombwa na uongozi wa Namungo FC kusalia klabuni hapo huku mazungumzo ya kumpa ofa nyingine yakitegemewa kuanza hivi karibuni na anatakiwa awepo hapo kwani ligi kuu itaanza Septemba 6 huku Namungo wakiwa na mchezo mwingine mgumu wa ngao ya hisani hapo tarehe 29 Agosti
Post a Comment
0
Comments
MERIDIAN BET
EURO 2024
Kuanzia tarehe 14 june to 14 july AMOSPOTIXTRA TEAM itakuwa ujerumani kukuletea michuano ya EURO2024
0 Comments