advertise with us

ADVERTISE HERE

KAULI YA MO DEWJI KUHUSU SENZO YAIBUA SHANGWE MSIMBAZI


Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi Simba Bw.Mohammed Dewji amewataka wanasimba wasisikitike kufuatia aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa timu hiyo Senzo Masingisa kutangaza kujiuzulu n kuhamia klabu ya Yanga

Ni siku mbili tu zimepita tangu Simba wamsajili Morrison kama mchezaji huruna Yanga wameamua kulipa kisasi kwa kumchukua CEO huyo wa mabingwa wa FA na Ligi kuu Tanzania Bara. Mo Dewji kupitia Twitter ameandika "Tumetoka mbali na bado safari inaendelea, tumepita mengi Wana Simbawenzangu. 

"Nawaomba WanaSimba wote mtulie. Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali Simba. Kazi inaendelea tuko imara,"

Kauli hiyo mepokelewa vyema na mashabiki wa klabu hiyo huku wengi wakisisitiza kushikamana na kushirikiana na timu hiyo ni kubwa kuliko mtu yeyote

Post a Comment

0 Comments