BETI NASI UTAJIRIKE

KAULI YA MANARA YAZIDI KUIMARISHA UKUBWA WA SIMBA


Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara anakuwa kiongozi wa wa pili wa Simba kutoka hadharani na  ambaye hajateteleka kuondoka kwa aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa klabu hiyo Senzo Mbatha . Manara amehojiwa na kituo kimoja cha redio na amenukuliwa akisema 

"Tumetoka mbali na bado safari inaendelea, tumepita mengi Wana Simbawenzangu.  Nawaomba WanaSimba wote mtulie. Simba ni kubwa kuliko mtu mmoja. Sisi viongozi tunawatumikia usiku na mchana bila kujali maslahi ya mtu binafsi bali Simba. Kazi inaendelea tuko imara,"

Manara ameendelea kusisitiza kuwa timu hiyo ni imara na hakuna wa kuitetelesha . Mbali na hayo msemaji huyo anaungana na mwekezaji na mwenyekiti wa bodi ya uwekezaji Simba Mohammed Dewji  kuwa kitu kimoja kuelekea msimu wa 2020/21

Post a Comment

0 Comments