advertise with us

ADVERTISE HERE

KAULI YA HAJI MANARA YAIBUA MAJONZI KWA MASHABIKI WA SOKA NCHINI


Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amefunguka rasmi kuwa atapumzika kidogo kuhusiana na masuala ya Simba na hoja kuu ni kuwa afya yake si imara kama awali. Manara amefunguka hayo wakati klabu hiyo ilipofanya dua maalumu ya kuiombea klabu hiyo kuelekea msimu wa 2020/21. 
Manara alinukuliwa akisema Afya yangu siyo sawasawa madhubuti labda mnaweza mkashangaa…Nisiwakwaze, mnaweza mkashangaa baada ya muda mchache ujao nikawaomba kupumzika na nitumie furusa hii kuwaambia nipo Simba nitawaomba Wanasimba nipumzike kidogo kwa sababu ya afya yangu siyo madhubuti sawasawa, nitaendelea kuhamasisha nje ya Simba. Asanteni sana,” -Amesema Haji Manara.

Kauli hii imepokelewa kwa masikitiko makubwa na mashabiki mbalimbali wa soka nchini huku wengi wakimtaka msemaji huyo kubakia katika nafasi hiyo ndani ya klabu ya simba . Sisi kama Amospoti tunatambua pumziko la manara litakuwa ni pigo kwa mashabiki wa soka si Simba tu bali kwa vilabu vyote kwani amekuwa akiufanya mpira kuwa kivutio na sisi kama wanahabari tunamuomba Manara aweze kubaki katika nafasi hiyo kwa sasa kwani nchi na ligi vinamhitaji.

Post a Comment

0 Comments