BETI NASI UTAJIRIKE

KAPTENI YANGA AFUNGUKA MIPANGO YAO MSIMU WA 2020/21


Kiungo kiraka Deus Kaseke amesema baada ya changamoto nyingi walizopitia msimu uliopita, msimu huu wamejipanga kufanya vizuri.Kaseke ambaye amepewa majukumu ya unahodha wakati huu akisubiriwa kocha mkuu, amesema kwa upande wake atahakikisha anaisaidia timu kufikia malengo

"Msimu mpya mara nyingi unakuwa na changamoto nyingi maana kila timu hujipanga kutokana na ushindani uliopo, nasi tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri"
"Binafsi, namuomba sana Mungu anisaidie maana natarajia kufanya vyema zaidi ya nilivyofanya msimu uliomalizila ili kuipa mafanikio timu yangu nje na ndani ya uwanja," alisema Kaseke

Kaseke ni mmoja wa wachezaji waandamizi waliobaki kwenye kikosi cha Yanga, pamoja na nyota kama Haruna Niyonzima na Said Juma Makapu

Post a Comment

0 Comments