INJINIA HERSI NDIYE MFALME MPYA WA YANGA


Habari ya mjini ni kwamba tayari wachezaji Tuisila Kisinda na Mukoko Tonombe waliokuwa wakisubiriwa kwa hamu, wamekanyaga ardhi ya Tanzania wakijiunga na mabingwa wa kihistoria, Yanga
Wachezaji hao wametua majira ya saa saba na nusu mchana wakiongozana na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said aliyewafuata kuwasajili huko huko Congo katika klabu ya AS Vita waliyokuwa wakicheza
Achana na mapokezi makubwa ya umati wa mashabiki waliojitokeza kuwalaki wachezaji hao, Injinia Hersi nae akakutana na sapraizi yake
Mwamba huyo aliyekonga nyoyo za mashabiki baada ya kukamilisha usajili wa wachezaji hao, aliandaliwa kiti maalum ambacho alikaa na mashabiki kumbeba juu juu kwa furaha huku wakiimba GSM...GSM...GSM..
Hili ni tukio la heshima kubwa ambalo mashabiki wa Yanga wamemfanyia Injinia na kampuni ya GSM kwa ujumla wakionyesha kutambua na kuthamini kile ambacho wanaifanyia klabu ya Yanga

Post a Comment

0 Comments