Klabu ya Ihefu FC imeendelea kujiandaa na msimu wa 2020-21 kwa kusajili wachezaji saba wapya kutoka vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania Bara.Ihefu msimu wa 2019/20 ilikuwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza na ilipanda kwa faida ya mabao mawili iliyopata ugenini ilipomenyana na Mbao FC kwenye mchezo wa playoffs Uwanja wa Kirumba.
Mchezo wa kwanza, Ihefu ilishinda mabao 2-0 kisha mechi ya pili ilikubali kichapo cha mabao 4-2 ila ilishinda kwa faida ya mabao ya ugenini kwa kuwa jumla walikuwa wamefungana mabao 4-4.
Hawa hapa wana uhakika wa kuwa ndani ya kikosi cha Ihefu msimu wa 2020/21- Agosti 17 walianza na beki wa kati Geoffrey Raphael Kivywanzi walinasa saini yake akitokea timu ya Mbeya Kwanza.
Pia Agosti 17 mshambuliaji wao ambaye ni kapteni, Joseph Kinyozi aliongeza dili la kubaki ndani ya Ihefu.
Agosti 18, mshambuliaji, Jordan John alisaini Ihefu akitokea Klabu ya Mbao FC.
Agosti 18 beki wa kati Wema Sadoki alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu alitokea Klabu ya Alliance FC.
Agosti 18, Kiungo wao, Willy Mgaya aliongeza mkataba wa kuendelea kuichezea timu hiyo.
Agosti 19, mshambuliaji, Paul Materaz Luyungu alisaini mkataba wa kuichezea timu ya Ihefu FC akitokea Klabu ya Lipuli.
Agosti 20, kiungo Omary Khamis alisaini mkataba wa kuitumikia timu ya Ihefu akitokea timu ya Ndanda FC.
Habari zinaeleza kuwa nyota wote hao kila mmoja amesaini dili la mwaka mmoja kupambania taji la Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.
0 Comments