BETI NASI UTAJIRIKE

IFAHAMU SAFARI YA VILABU 3 VILIVYOPANDA LIGI KUU TANZANIA BARA


Klabu ya Ihefu kutoka Mbalali jijini Mbeya imefanikiwa kupanda ligi kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza tangu kunzishwa kwake. Klabu hiyo imepanda daraja mara baada ya kutoka sare ya mabao 4-4  dhidi ya mbeya City.

1.IHEFU 
Mchezo wa kwanza kati ya Ihefu na Mbao ulichezwa jijini mbeya (nyumbani kwa Ihefu) na ulimalizika kwa Ihefu kushinda mabao 2-0 . Mchezo wa marudiano ulipigwa hapo jana tarehe 01 nyumbani kwa Mbao FC na ulimalizika kwa Mbao kushinda mabao 4-2 hivyo kufanya timu hizo kuwa zimefungana jumla ya mabao 4-4. 

Ihefu ilinfaika na bao la ugenini na kuifanya iwe na mabao 5-4 dhidi ya Mbao. Kwa matokeo hayo  Ihefu inapanda ligi huku Mbao ikishuka daraja la kwanza.


2. GWAMBINA FC 
Klabu ya Gwambina FC ilifanikiwa kupanda ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuwa na pointi nyingi kwenye kundi A ligi Daraja la kwanza. Matokeo yale yaliifanya ifuzu moja kwa moja ligi kuu huku nafasi ya pili ikiwa ni Geita Gold iliyoshindwa kupanda daraja baada ya kutolewa na Mbeya City kwenye mchezo wa PLAY OFF 



3. DODOMA JIJI FC 
Timu ya jiji la Dodoma wao walifaniiwa kupanda ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuwa na pointi nyingi kwenye kundi B ligi daraja la kwanza. Matokeo mazuri yaliifanya Dodoma FC ifuzu moja kwa moja ligi kuu Tanzania bara huku nafasi ya pili ikiwa ni hefu iliyofanikiwa kupanda pia baada ya kuishinda Mbao FC 



Post a Comment

0 Comments