BETI NASI UTAJIRIKE

IBRAHIM AJIBU WA MWAKA 2020 ATAKUWA BORA ZAID


Ibrahim Ajibu ni mchezaji mwenye jina kubwa sana hapa nchini. Jina halikuja kwa bahati mbaya, ana kipaji kikubwa
Mashabiki wana matumaini makubwa kwake, wengi wakiamini kwa uwezo alionao, pengine alipaswa kuwa walipo akina Mbwana Samatta
Msimu wake wa kwanza baada ya kurejea Simba akitokea klabu ya Yanga haukuwa mzuri
Ajibu alikumbana na changamoto za hapa na pale akikosa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza
Katika makocha wengi ambao wamemzungumzia Ajibu, hakuna hata mmoja ambaye alikataa kipaji chake, wengi walikosoa utaratibu wake wa kufanya mazoezi
Hata Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alisema kuwa Ajibu ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini anapaswa kuongeza juhudi ya mazoezi ili ajihakikishie nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza
Kwa usajili uliofanywa na Simba, ni wazi Ajibu anapaswa kujituma kwelikweli ili apate nafasi
Alianza vizuri kwenye mchezo wa Simba Day akifunga bao katika ushindi wa mabao 6-0, akionyesha kiwango kizuri pia
Mwenyewe amesema msimu huu hatakuwa na maneno mengi, muda ndio utakaozungumza

Post a Comment

0 Comments