Klabu ya Simba imefanikiwa kumnasa aliyekuwa beki wa Coastal Union Ibrahim Ame. Simba ni kama wamefikia hatua ya kulipiza kisasi kwa Yanga baada ya kumkosa beki waliyekuwa wanampigia hesabu kumnasa Bakari Mwamnyeto. Ame na Mwamnyeto walikuwa nguzo imara ya ulinzi kwa Coastal Union msimu wa 2019/20 baada ya kufungwa mabao 30 tu huku timu hiyo ikishika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi uliomalizika . Inasemekana Ame amesaini mkataba wa miaka 2 ndani ya Simba huku Bakari Mwamnyeto akisaini Yanga kwa miaka miwili pili. Kwa mashabiki wa soka wanasema usajili huo utanogesha dabi y Simba na Yanga kutokana na mabeki hao mahili kuwa timu mbili tofauti tena zenye utani wa jadi. Swali linabaki kwa mashabiki kuwa ni nani atakuwa zaidi ya mwenzake msimu ? tusubiri ligi ianze mwezi septemba tarehe 06
0 Comments