advertise with us

ADVERTISE HERE

HIZI NI SABABU MBILI ZA IKER CASSILAS KUTUNDIKA DARUGA


Aliyekuwa Golikipa wa Hispania,Real Madrid na FC Porto Iker Cassilas ametangaza rasmi kutaafu soka baada ya kuwa uwanjani kwa miaka 22 akicheza michezo 725 kwa timu ya taifa na vilabu hivyo viwili alivyovitumikia.

Cassilas amestaafu soka akiwa na umri wa miaka 39 huku akiweka rekodi ya kushinda ubingwa wa ulaya mara tatu ndani ya Real Madrid, Ubingwa wa La Liga mara tano na ubingwa wa Ureno mara tatu. Kombe la dunia mara 1 mwaka 2010 na ubingwa wa EURO 2008 na ule wa 2012 

Cassilas amefikia hatua baada ya kuwa na shambulio la moyo alilolipata mwaka 2019 kabla ya ligi kuanza na ilitegemewa angestaafu mwaka huo lakini alijumuishwa kwenye kikosi cha porto kilichocheza msimu wa 2019/20.

Inasemekana mara baada ya kustaafu atagombea nafasi ya urais kwa chama cha Soka Uhispania (Spanish Football Federation). Mbali na mipango hiyo ya kugombea uraisi lakini pia ametajwa kuwa moja ya viongozi wajao kwa klabu ya Real Madrid .

Cassillas ni kipa nambari moja duniani kwa karne ya 21 akiwa ameshinda tuzo ya kipa bora duniani mara 5 , kutajwa kikosi bora cha dunia mara 5 kutwaa ukipa bora kwenye michuano ya EURO,kombe la dunia ,La Liga na hata UEFA . 

Taarifa za kustaafu kwake aliziweka kupitia mtandao wa kijamii na baadhi ya mashabiki wamehuzunishwa na kuondoka kwa nyota huyo makini zaidi kwenye historia ya soka la hispania na dunia kwa ujumla.

Post a Comment

0 Comments