advertise with us

ADVERTISE HERE

HISTORIA YA ELCHE INASISIMUA ,WAMEREJEA LA LIGA KIBABE,


Bao pekee alilofunga Pere Milla limeisaidia klabu ya Elche kurejea ligi kuu Hispania maarufu kama  La Liga baada ya kuifunga Girona 1-0. Shukrani kwa Pere aliyefunga bao la kichwa dakika za nyongeza kwenye mchezo huo wa pili baada ya ule wa kwanza uliopigwa kumalizika kwa sare ya 0-0.

Elche wanarejea rasmi La Liga baada ya kukosekana kwa misimu mitano na walishuka daraja msimu wa 2014-15.Klabu hiyo ilishuka daraja ikiwa nafasi ya 13 na sababu kubwa ya kushushwa ni ukata wa fedha ndani ya timu hiyo na  iliyokuwa timu ya kwanza duniani kushuka daraja kwa matatizo ya kiuchumi.

Tangu kushuka ligi daraja la pili iliendelea kuporomoka mpaka ligi daraja la tatu.Kwa sasa klabu hiyo imerejea La Liga ikiungana na Huesca pamoja na Cadiz iliyomaliza nafasi ya pili


Post a Comment

0 Comments