Hapo jana usiku wa tarehe 7 ilikuwa ni siku mahususi kwa mashabiki wa soka la Tanzania kushuhudia wachezaji,Viongozi pamoja na timu mbalimbali zilivyofanya vyema msimu wa 2019/20. Clatous Chama na klabu yake ya Simba walifanikiwa kufunika tuzo hizo
Chama alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu na kiungo bora wa msimu huku klabu ya Simba ikiondoka na dau nono la milioni 100 lililokabidhiwa na Vodacom wadhamini wakuu wa ligi kuu
Hii ni Orodha ya wachezaji ,Timu,Marefa waliotwaa tuzo hizo
Bingwa wa VPL-Simba SC (Dar Es Salaam)
Mshindi wa pili VPL-Yanga SC (Dar Es Salaam).
Mshindi wa tatu VPL-Azam FC (Dar Es Salaam).
Mshindi wa nne VPL-Namungo FC (Lindi)
Timu yenye Nidhamu bora-Kagera Sugar (Kagera).
Mwamuzi bora Msaidizi-Frank Komba (Dar Es Salaam).
Mwamuzi bora wa kati-Ramadhan Kayoko (Dar Es Salaam).
Mfungaji bora-Medie Kagere (Simba SC).
Kocha Bora-Sven Vandenbroeck (Simba).
Golikipa bora-Aishi Manula (Simba).
Mchezaji bora Chipukizi- Novatus Dismas (Biashara United).
Beki bora-Nicolaus Wadada (Azam FC)
Kiungo bora-Clatous Chama (Simba).
Tuzo Maalumu-Sunday Ramadhan Manara (Dar Es Salaam).
Goli bora la Msimu-Patson Shikala (Mbeya City)-Mechi ya Mbeya City vs JKT Tanzania.
Mchezaji bora wa msimu wa VPL 2019/2020-Clatous Chota Chama (Simba).
0 Comments