advertise with us

ADVERTISE HERE

DAU LA MORRISON NDANI YA SIMBA NI KUFURU


Aliyekuwa kiungo  mshambuliaji wa klabu ya Yanga Benard Morrison amejiunga rasmi na mabingwa wa wa FA na ligi kuu msimu wa 2019/20 klabu ya Simba. Mbali na kwamba uogozi wa Yanga kudai una mkataba na mchezaji huyo ila ukweli ni kuwa mchezaji huyo hakusaini mkataba huo.

Morrison alijiunga na Yanga kipindi cha dirisha dogo la usajili kwa mkataba wa miezi 6  na Julai 14 mkataba wake na Yanga ulimalizika lakini uongozi wa Yanga wanadai mchezaji huyo bado ni mali yao na anamkataba wa miaka miwili na klabu hiyo kongwe ,Suala la mchezaji huyo na Yanga lipo kamati ya maadili TFF na hivi karibuni taarifa rasmi itatolewa.

Morrison anakuwa ni mchezaji wa tatu kusajiliwa ndani ya Simba.huku Ilanfya akishika nafasi ya kwanza na Ibrahim Ame alikuwa wa pili kusajiliwa huku Morrison akiwa mchezaji wa tatu kusajiliwa. 

Inasemekana Morrison alinunuliwa kwa milioni 150 huku akipewa mshahara mnono kwa kipindi cha miaka miwili ya kuitumikia Simba

Post a Comment

0 Comments