Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa Burundi Kaze Cedric ametajwa kuwa ndiye mrithi wa Luc Eymael aliyetimuliwa nchini mwezi Julai kwa madai ya kauli za kibaguzi alizozitoa dhidi ya mashabiki wa Yanga.
Cedric Kaze amekuwa gumzo kwa soka la Africa Mashariki kwani anamiliki leseni ya daraja la kwanza CAF pamoja na leseni ya Chama cha soka Ujerumani Deustcher Fussball Band (DFB).
Wasifu wa kocha huyo
1. Kocha mkuu wa timu ya taifa Burundi U17,U20,U23 na timu ya taifa
2.Amefanya kazi kwenye akademi ya Barcelona
3.Amefundisha timu ya FC Edmonton inayoshiriki ligi kuu Canada.
4.Amesoma shule ya Hennef Sports School huko ujerumani na ndiko alikopata leseni yake.
Cedric Kaze amewahi kuwafunga Yanga mabao 2-0 wakati akiifundisha Atletico Olympic walipokutana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho mwaka 2012 jijini Dar es Salaam
0 Comments