BETI NASI UTAJIRIKE

CLATOUS CHAMA AFUNGUKA BAADA YA KUTWAA TUZO


Nyota wa Zambia anayekipiga Simba Clatous Chama amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora na kukabidhiwa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Shirikisho. 

Simba imetwaa taji mbele ya Namungo FC kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kibabe uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela,  Sumbawanga. 

Mabao ya Simba yalifungwa na Luis Miqussone na John Bocco na lile la Namungo lilifungwa na Edward Manyama.Chama ndani ya Simba ni kinara wa kutupia mabao akiwa nayo manne na pasi tatu za mabao.

Chama amesema:"Furaha kubwa katika hili kwa kuwa ilikuwa ni kazi ngumu ila tumefanikiwa kwa kuwa sisi sote ni timu moja.

Post a Comment

0 Comments