CHUMA HIKI CHA KMC KINAPIGIWA HESABU NA SIMBA


Klabu ya KMC imefikia makubaliano ya kumuachia nyota wao Charles Ilanfya kwenda Klabu ya Simba SC inayonolewa na Sven Vandenbroeck.Mshambuliaji huyo mzawa ambaye amekuwa bora mwishoni mwa msimu baada ya kuanza kwa kusuasua kwa kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya nyama alikuwa kwenye rada za Yanga pia.

Aliibuka ndani ya KMC msimu wa 2018/19 akitokea Klabu ya Mwadui FC ambapo alivunja mkataba huko kutokana na ishu ya kutolipwa stahiki zake.Ilanfya amesema kuwa hana hiyana iwapo itatokea Simba ama Yanga zikahitaji saini yake kwa kuwa ni mchezaji.

"Sina presha na uwezo wangu ikitokea Simba ama Yanga wakahitaji saini yangu sina tatizo nitafanya kazi ila kwa sasa bado nipo ndani ya KMC," amesema.
Habari kutoka ndani ya KMC zinaeleza kuwa wamewaambia Simba kwamba iwapo wanahitaji saini ya nyota huyo ni suala la kukaa mezani.

Post a Comment

0 Comments